Mshiriki wa mbio za Baiskeli wanawake, Alavuya Ntalima akishangiliwa na
wanamichezo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati alipokuwa anawasili baada
ya kushiriki mbio za Kilomita 32 za Baiskeli kutoka Kijiji cha Melela Mlandizi
hadi Rombo mjini Morogoro. Timu 12 za Baiskeli za Shirikisho za Michezo ya
Wizara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI)
zilishiriki katika mbio hizo leo. Hata hivyo, Timu za mpira wa miguu, Kamba
wanaume na wanawake na Netball zimeingia katika kundi la 16 Bora huku Timu ya
mchezo wa riadha mita 100 ya wizara hiyo imeingia fainali.
|
No comments:
Post a Comment