WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 6 October 2014

TIMU ZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI ZAONGOZA UFUTAJI WA KAMBA SHIMIWI MOROGORO

Timu ya wavutaji kamba wanaume ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwavuta wapinzani wao (hawapo pichani) Wizara ya Ujenzi wakati walipokuwa wanashindana katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro leo. Timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliibuka mshindi kwa pointi moja.
Timu ya wavutaji kamba wanawake ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwavuta wapinzani wao (hawapo pichani) Wizara ya Afya wakati walipokuwa wanashindana katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro leo. Timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliibuka mshindi kwa pointi zote mbili.
Muhamasishaji wa uvutaji kamba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Salma Hamza (katikati) akilia kwa furaha baada timu zote mbili za wizara hiyo kuibuka kidedea katika mashindano ya uvutaji kamba katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara pamoja na Taasisi zake (Shimiwi) yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa Timu ya Netball ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dafroza Benard (kulia) akiuangalia mpira aliourusha ukiingia katika nyavu ya timu ya Wizara ya Afya wakati walipokuwa wakicheza na timu hiyo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment