WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Sunday, 20 July 2014

WAZIRI CHIKAWE ASHIRIKI MAZISHI YA MZAZI WA DIWANI NACHINGWEA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) na waombolezaji wakiswalia mwili wa marehemu ambaye ni mama mzazi wa Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea,  Sada Makota. Mazishi ya Mama Mzazi wa Diwani huyo yamefanyika katika Kijiji cha Nangunde, Kata ya Namikango wilayani Nachingwea leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akimfariji Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Sada Makota kwa kufiwa na mama yake mzazi, wakati alipofika nyumbani kwa Diwani huyo wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika katika Kijiji cha Nangunde, Kata ya Namikango wilayani Nachingwea leo.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya Mama Mzazi wa Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Sada Makota, wakati alipofika nyumbani kwa Diwani huyo katika Kijiji cha Nangunde, Kata ya Namikango wilayani Nachingwea leo.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (aliyevaa Miwani) akiwa na waombolezaji wa msiba wa Mama Mzazi wa Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Sada Makota. Mazishi ya Mama Mzazi wa Diwani huyo yamefanyika katika Kijiji cha Nangunde, Kata ya Namikango wilayani Nachingwea leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri Chikawe amwaga misaada ya mabati 100 na jezi za mipira Nachingwea

Felix Mwagara, Nachingwea
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe ametoa msaada wa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Nditi pamoja na jezi za mpira wa miguu kwa timu sita zilizopo katika kata hiyo, jimboni kwake Nachingwea mkoani Lindi jana.
Waziri Chikawe pia ametoa mifuko 15 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti uliopo katika Kata hiyo pamoja na kuwataka wananchi washirikiane kufanya kazi ili kuiletea maendeleo kata yao ambayo ni moja ya kata ni muhimu katika Jimbo lake la Nachingwea.
Akizungumza baada ya kutoa msaada huo pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za viongozi wa Kata ya Nditi katika mkutano na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata hiyo, Wajumbe wa Mabaraza wa Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee wa Kata alisema chama chake CCM kipo bega kwa nega na wananchi ikiwa na lengo la kuwaletea maendeleo zaidi.
“Nafurahi leo (jana) kuzungumza na viongozi wa Kata hii, nimekuja hapa kusikiliza kero zenu ambazo mnazijua ndani ya kata hii, hata hivyo nimezisikiliza kupitia hotuba yenu pamoja na maswali mbalimbali mlioniuliza, na tayari baadhi ya maswali yenu nimeyajibu na mlichokuwa mnahitaji nimewasaidia,” alisema Chikawe.
Chikawe aliongeza kuwa, licha ya kuendelea kutoa misaada ya kijamii mbalimbali katika jimbo lake lakini pia amepanga kukuza michezo katika jimbo hilo ambapo ameanza kwa kutoa msaada wa jezi kwa timu sita za mpira wa miguu katika Kata ya Nditi na baadaye atahamia katika kata zingine za jimboni kwake.
“Michezo ni muhimu kwa afya na pia muhimu kwashughulisha vijana hawa, maana kuna msemo usemao ‘Usipowashughulisha vijana hawa watakuja kukushughulisha, sasa ngoja tuwashughulishe kabla ya kutushughulisha,” alisema Chikawe.
Akizungumza baada ya kupokea msaada wa jezi za mpira wa miguu, Afisa Mtendaji wa Kata ya Nditi, Patrick Mwasambungu alimshukuru Waziri Chikawe kwa msaada huo na jezi hizo atazigawa kwa timu hizo katika kata yake.
Aidha, Chikawe aliwataka viongozi hao kutoa elimu zaidi kwa wananchi wao endapo rasimu ya pili ya Katiba ikipitishwa na Bunge la Maalum la Katiba washiriki kikamilifu katika kupiga kura ya maoni kwani Katiba ndio msingi wa maisha ya kila Mtanzania na muelekeo wa nchi yetu. 
Waziri Chikawe yupo jimboni kwake Nachingwea kwa ziara maalum ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika kata zake pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowasibu katika kata zao.
Mwisho/-

CHIKAWE AMWAGA MISAADA YA MABATI NA JEZI ZA MIPIRA JIMBONI KWAKE


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akimkabidhi jezi za timu sita za mpira wa miguu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nditi, Patrick Mwasambungu kwa ajili ya kuzikabidhi timu hizo zilizopo katika Kata hiyo katika Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe pia alitoa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikiangalia kifusi cha mchanga kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni akifanya  ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika Kata za Wilaya za Nachingwea mkoani Lindi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Nditi, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo ya Nditi wakati alipofanya ziara katika kata hiyo iliyopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe alitoa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Picha zote na Felix Mwagara.