WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 19 June 2015

WADAU WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA YANAYOENDELEA KATIKA VIWANJA VYA MJAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM

Askari wa Jeshi la Polisi, ASP Gabriel Mwasile (kushoto), akitoa maelezo kuhusu sare iliyokuwa inavaliwa na askari wa kike,  kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 Kamishna wa Uhamiaji (Sheria), Said Kamugisha , akisaini kitabu alipowasili katika banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kushiriki katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Violet Mwangalaba na Felix Mwagara wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
 Afisa Probeshini na Huduma kwa Jamii, Pendo Mtama akitoa maelezo kuhusu huduma za Probesheni na Huduma kwa Jamii  kwa Kamishna wa Uhamiaji (Sheria), Said Kamugisha aliyeshiriki katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Afisa Tawala, Idara ya Wakimbizi, Jeremia Chuma akitoa maelezo kwa Kamishna wa Uhamiaji (Sheria), Said Kamugisha, kuhusu huduma zinazotolewa kwa wakimbizi nchini, wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Dar es Salaam.
 Wadau wakiangalia vielelezo katika banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmmoja jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment