WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday 4 September 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MFUMO WA TAKWIMU HURIA BARANI AFRIKA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (kulia meza kuu) katika Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ili aweze kuufungua mkutano huo. Katika hotuba yake Waziri Chikawe alisema mfumo wa utoaji taarifa kwa uwazi umekuwa muhimu kwani unaleta uwazi pamoja na uwajibikaji katika utoaji wa huduma. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 Afrika, unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika. Wapili kulia meza kuu, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird. Anayefuata ni Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa makini wakati akitoa hotuba yake katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 barani Afrika unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani humo. 
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 Afrika, unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika. Wenyeji wa mkutano huo ni Serikali ya Tanzania wakishirikiana na Benki ya Dunia.

Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika ndege ambayo inapaa bila rubani (Drone) na yenye uwezo wa kuchukua matukio mbalimbali ikiwa angani, wakati alipotembelea Banda la Buni Hub ambalo lipo chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mtaalamu wa Benki ya Dunia, Frederick Mbuya akitoa elimu ya ndege hiyo kwa Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia kwa Rais Kikwete) pamoja na viongozi wengine walioambatana na Rais huyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment