WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Saturday, 17 October 2015

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAMBI YA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akizungumza na uongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma alipofanya ziara wilayani humo kwa ajili ya kukagua Kambi ya Nduta wilayani humo pamoja na Kambi za Mtendeli na Karago wilayani Kakonko ambazo zipo katika maandalizi ya kuwapokea wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa kwa muda katika Kambi ya Nyarugusu mkaoni humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.

Mhandisi wa Maji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Msafiri Mtyaule akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) kuhusu kisima ambacho kitasambaza maji kwa ajili ya wakimbizi kutoka Burundi ambao watahifadhiwa katika Kambi ya Mtendeli wakitokea Kambi ya Nyarugusu ambapo wanahifadhiwa kwa muda. 
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, Fred Nisajile akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) moja wapo ya madarasa yatakayotumiwa na wakimbizi watakaohamishiwa katika Kambi ya Karago kutoka Kambi ya Nyarugusu wanapohifadhiwa kwa muda. Ubaoni ni picha na maandishi yaliyoachwa na wakimbizi walioishi katika kambi hiyo kabla ya kufungwa mwaka 2007.

Baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi wakipokelewa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta. Idadi ya wakimbizi kutoka nchini humo inazidi kuongezeka siku hadi siku.

Askari Polisi wanaosimamia usalama katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wakikagua mizigo ya wakimbizi kutoka Burundi wanaopokelewa katika kambi hiyo ili kuhakikisha usalama wa mizigo yao.

Watoto wa Wakimbizi kutoka Burundi wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta ambapo wanahifadhiwa.

Baadhi ya mahema yanayojengwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma ambayo yatatumika kuwahifadhi wakimbizi kutoka Burundi wanaoendelea kuwahamishiwa kambini hapo kutoka Kambi ya Nyarugusu ambapo walikuwa wamehifadhiwa kwa muda.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.      

No comments:

Post a Comment