Katibu
Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akizungumza na
wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa
siku moja wa baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Jeshi la Magereza,
Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, John Mngodo, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga.
Wapili kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu
Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone. Katika kikao hicho Abdulwakil aliwataka
watumishi wa wizara yake wafanye kazi kwa uadilifu na weledi ili kuleta
mafanikio ndani ya wizara hiyo muhimu katika maendeleo ya nchi.
|
No comments:
Post a Comment