WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday 18 December 2015

WAZIRI KITWANGA ALA KIAPO CHA KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya kumuapisha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (katikati), mara baada ya Jaji huyo kumuapisha Waziri Kitwanga kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu wa Waziri huyo, Nelson Kaminyoge.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akipandisha ngazi za kuingia Mahakama Kuu wakati alipokuwa anaenda kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza. Jaji Kiongozi wa Mahakama hiyo, Shabani Lila alimuapisha Waziri Kitwanga Mahakamani hapo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Waziri Kitwanga kuapishwa na Jaji huyo kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza katika tukio lililofanyika Mahakamani hapo, jijini Dar es Salaam leo.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu nchini, Shabani Lila (katikati) akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) mara baada ya kumaliza kumuapisha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Kushoto ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.

No comments:

Post a Comment