Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi
la Polisi nchini. Waziri Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa,
wamekubaliana na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo kuweka mikakati zaidi ya
kukabiliana na uhalifu nchini. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Wapili kulia meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam
Kaniki. Kulia ni Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul
Chagonja. Kushoto meza kuu ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Mussa Ali Mussa.
Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa
Jeshi la Polisi, Suleiman Kova.
|
No comments:
Post a Comment