WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Thursday 17 December 2015

WAZIRI KITWANGA AANZA ZIARA ZAKE KWA KUTEMBELEA JESHI LA POLISI, AWATAKA MAKAMANDA NA ASKARI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) wakati alipokitembelea kituo hicho cha Polisi jijini Dar es Salaam leo. Pia Waziri Kitwanga katika ziara yake hiyo ya kwanza tangu alipoteuliwa kuiongoza wizara hiyo, alitembelea Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), pamoja na kukagua nyumba za Makazi ya Polisi za sasa na zamani zilizopo barabara ya Kilwa. Wanne kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akitoka kuikagua moja ya nyumba ya zamani ya Jeshi ya Polisi ambayo inakaliwa na baadhi ya askari iliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Waziri Kitwanga alizikagua nyumba hizo za zamani pamoja na zakisasa zilizopo katika eneo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiiangalia nyumba ya mabati ya makazi ya Polisi wakati alipoingia ndani huku akitokwa na jasho kutokana na joto kali ndani ya nyumba hiyo. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kutembelea nyumba hizo zilizopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na kushoto ni  mkazi wa nyumba hiyo, ambaye ni askari Polisi, Nelson Chale.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kushoto) wakizikagua nyumba za kisasa ambazo ni za ghorofa za Jeshi ya Polisi nchini zilizopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara kuzitembelea nyumba hizo ili kujionea ukosefu wa nyumba unaowakabili Polisi nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), akiwauliza maswali Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Kamishina Thobias Andengenye (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), DCP Ally Lugendo wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika Chuo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akimsikiliza kwa makini Mkufunzi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), Inspekta Novatus Akondowe (kulia) alipokuwa anamuuliza swali. Waziri Kitwanga alitoa ruhusa ya kila mkufunzi wa chuo hilo waeleze matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo chuoni hapo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari alioambatana nao wakati wa ziara yake katika Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo jijini Dar es Salaam. Pia Waziri huyo katika ziara yake hiyo ya kwanza tangu alipoteuliwa kuiongoza Wizara hiyo, alitembelea nyumba ya Makazi ya Polisi barabara ya Kilwa, Kituo Kikuu cha Polisi (Central), Kituo cha Polisi Msimbazi na Kituo cha Polisi Oysterbay.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai), Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Kamishina Thobias Andengenye (kulia) na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), DCP Ally Lugendo (wapili kulia) wakikwepa waya wakati walipokuwa wanamuonyesha Waziri Kitwanga mabweni ya Chuo hicho kilichopo barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akilikagua moja ya darasa linalotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA). Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kukitembelea chuo hicho pamoja na kuzungumza na wakufunzi wa chuo hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akionyeshwa moja ya gari la maji washa, na Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova katika Kambi ya Jeshi la Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo.


No comments:

Post a Comment