WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 11 December 2015

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MAFUNZO YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHUO CHA UONGOZI JKT KIMBIJI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akisalimiana na Uongozi wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji pamoja na Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipowasili Chuoni hapo kufunga mafunzo ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kozi ya Awali  yaliyofanyika hayo Chuoni hapo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyofanyika katika Chuo cha yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji, jijini Dar es Salaam.

 Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo yaKozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likipita mbele ya mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.

Muhitimu wa Mafunzo ya Kozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Semeni Daudi Chiunda, akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, kutokana na kuwa Mhitimu Bora katika kipingere cha Ukakamavu wakati wote wa Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment