WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Saturday, 12 December 2015

WAZIRI KITWANGA AKARIBISHWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MARA BAADA YA KUAPISHWA IKULU, DAR ES SALAAM LEO


Rais Dkt. John Magufuli (kushoto) akimuapisha Charles Kitwanga (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ikulu jijini Dar es salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo mara baada ya kumpongeza Waziri huyo mpya, nje ya Ukumbi wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia) akimkaribisha wizarani Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya kuapishwa Ikulu, jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimkaribisha Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ndani ya ofisi ya waziri huyo iliyopo Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha wageni kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya Waziri huyo mpya kuingia ndani ya ofisi hiyo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto) akimfafanulia Waziri mpya wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kulia), shughuli mbalimbali zinazofanywa na wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akijadiliana na watendaji wa wizara hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (D/IGP), Abdurahman Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja (hayupo pichani). Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.


No comments:

Post a Comment