WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 15 December 2015

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, ALITAKA JESHI LA MAGEREZA KUPUNGUZA MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI YASIYO YA MUHIMU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. John Mngodo akihutubia Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza lililofanyika leo Desemba 15, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa  Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali hapa nchini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi  Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza lililofanyika leo Desemba 15, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa yote Tanzania Bara, Makao Makuu ya Jeshi hilo, Wakuu wa Vyuo vya Magereza wakifuatilia majadiliano katika Baraza hilo.

Wajumbe wa  Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa wameshikana mikono huku wakiimba wimbo Maalum wa Mshikamano Daima “SOLIDARITY FOREVER”.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. John Mngodo akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa  Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza(walisimama). Wa Pili kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza, Haikamen Mshida(Picha zote na Lucas mboje wa Jeshi la Magereza).


No comments:

Post a Comment