WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 14 December 2015

WAZIRI KITWANGA, NAIBU WAZIRI WA USALAMA WA RAIA WA CHINA WASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) na Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang wakisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa Raia kati ya Wizara hizo mbili, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), wakibadilishana Hati za Makubaliano ya Ushirikiano waliosaini na Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akimpa zawadi ya kinyago Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, mara baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, kabla ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimpa maelezo mafupi Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (wapili kushoto), kabla ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Ndani nchini China, Zhang Xiaohui.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watano kulia-mstari wa mbele),  Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (watano kushoto-mstari wa mbele), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kulia-mstari wa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mawaziri hao kumaliza kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Tukio hilo lilifanya katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang, mara baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara hizo mbili. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment