WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 22 December 2015

WAZIRI KITWANGA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwasili Makao Makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kinondoni jijini Dar es Salaam na kupokewa na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu (kushoto). Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiieleza jambo menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil, wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo, na watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo.  Watano kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil, wanne kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo.
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Brenda Joshua akimfafanulia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai), jinsi wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri Kitwanga alitembelea Kituo hicho cha Usajili na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia kwa Abdulwakil ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment