WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday, 30 December 2015

WAZIRI MKUU AHITIMISHA ZIARA MKOANI KIGOMA,ATEMBELEA KAMBI ZA WAKIMBIZI, AWAONYA KUTOJIHUSISHA NA UHALIFU

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimzungumza na watumishi wa Serikali na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika Ukumbi wa NSSF mjini humo. Majaliwa aliwataka watumishi wa mkoa huo wafanye kazi kwa juhudi ili kuuletea maendeleo zaidi mkoa huo. Waziri Mkuu Majaliwa,  pia aliwaonya wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu na Nduta kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika kambi hizo . Kulia meza kuu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi mkimbizi Cesiwa Angelani (kushoto) zawadi ya ndoo yenye vifaa vya kumuhudumia mtoto baada ya mzazi huyo kujifungua katika Hopsitali iliyopo katika ya Nyarugusu ambapo Wakimbizi wanahifadhiwa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu (hawapo pichani) wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma, wakati alipofanya ziara ya kutembelea kambi za wakimbizi mkoani humo. Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
Sehemu ya Wakimbizi wa Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani)  wakati alipokuwa akizungumza na wakimbizi hao. Majaliwa aliwaonya wakimbizi hiyo kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika kambi hiyo.

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara katika kambi hiyo. Katika hotuba yakekwa wakimbizi wa kambi hiyo, Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akimwagilia mti wa kumbukumbu alioupanda katika Kambi ya Nduta,  Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wakati Waziri huyo alipoambatana  na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa katika ziara katika kambi hiyo. Katika hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa.

Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, wilayani Kibondo, Fred Nsijile akitoa taarifa ya kambi yake kwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto). Katika taarifa hiyo Mkuu wa Kambi alisema kambi yake inakabiliwa na upungufu wa maji kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoishi kambini humo. Hata hivyo katika hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa alisema atalifanyia kazi tatizo hilo na pia aliwaonya wakimbizi katika kambi hiyo kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa. Wapili kushoto meza kuu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (watatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke.
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akiwafurahia wacheza ngoma  ambao ni wakimbizi kutoka Burundi wakati walipokuwa wanamkaribisha katika Kambi ya Nduta, mkoani Kigoma kuzungumza na wakimbizi hao. Katika hotuba yake, Majaliwa aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika eneo waliohifadhiwa. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


No comments:

Post a Comment